Author: Admin

Bi. Stamili Endelea Kaloloma ambaye ni kikongwe wa miaka 119, mkazi wa Misegese wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro, ametelekezwa na watoto wake wapatao watano ambao hawataki kumtunza wala kumpatia mahitaji yake muhimu licha ya kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kupewa maagizo ya kumtunza kutokana na umri wake, badala yake wamemuacha apambane mwenyewe. Hali hiyo imemfanya […]

Vyombo vya habari nchini Korea Kaskazini, jana Jumapili, Januari 21, 2024 vimeripoti kuwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin anatarajiwa kuitembelea nchi hiyo hivi karibuni, kwa mwaliko wa Rais Kim Jong Un, hatua inayotajwa kuwa ni ishara kwamba ushirikiano kati ya viongozi hao wawili unaongezeka wakati vita vikiendelea nchini Ukraine na machafuko yakiongezeka Mashariki ya Kati. […]

MRITHI wa mikoba ya mshambuliaji, Jean Baleke ambaye anaondoka akiwa namba moja kwenye utupiaji ndani ya ligi akiwa katupia mabao 8, Michael Fred ana balaa kutokana na rekodi zake. Ni Michael Fred raia wa Ivory Coast anatajwa kubeba mikoba ya Baleke ambaye hatakuwa ndani ya kikosi cha Simba kwa msimu wa 2023/24 kwenye mechi zilizobaki […]

Kocha wa timu ya taifa ya Senegal, Aliou Cisse alipata matatizo ya kiafya, akawahishwa hospitalini kufuatia ushindi dhidi Cameroon, lakini sasa anaendelea vyema baada ya matibabu. Senegal waliendeleza mwanzo mzuri wa kutetea taji lao la Mataifa ya Afrika kwa ushindi wa mabao 3-1 na kutinga kibabe hatua ya 16 Bora. Hata hivyo Cisse alipata tatizo […]

MTANDAO wa Bayoanuai Tanzania umeshauri wakulima kulinda na kuendeleza kilimo cha asili ili kuendelea kuwa na uhuru wa matumizi ya mbegu za asili kwa usalama wa chakula na lishe. Mtaalam wa Mbegu kutoka katika mtandao huo, David Manongi amesema hayo katika warsha ya mbegu asili iliyofanyika mkoani Dar es Salaam. Amesema mbegu za asili ni […]

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi,ACP Janeth Magomi, amewaonya madereva kuacha tabia ya kuchezea mfumo wa Vehicle Truck Syteam  (VTS) kwani mfumo huo umewekwa kwa lengo mahususi la kusoma na kubaini mwendokasi wa magari ambapo kitendo cha kufanya hivyo ni kosa na atakaebainika atachukuliwa hatua za Kisheria. Kamanda Magomi ametoa onyo […]

Kocha mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha baada ya kutoka Ligi ya Mabingwa, leo atakuwa na mtihani mwingine kwenye Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar utakaochezwa leo saa 10:00 jioni katika uwanja wa Uhuru. Benchikha amekaa benchi kwenye mechi mbili za Simba dhidi ya Jwaneng Galaxy 0-0 na Wydad ambayo walifungwa 1-0. Katika mechi hizo […]

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Jenista Mhagama. ametoa wito kwa watumishi walio chini yake kufanya kazi kwa kutegemeana na kushirikiana bila kutengeneza makundi. Ametoa rai hiyo mkoani Morogoro wakati akifungua kikao cha baraza la wafanyakazi la Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na uratibu kilicholenga kujadili taarifa ya bajeti […]

Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kupitia kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itifaki na Mambo ya Nje John Mrema kimethibitisha kupokea hukumu iliyotolewa Alhamisi tarehe 14 Disemba, 2023 uamuzi wa Mhe. Jaji Cyprian Phocas Mkeha juu ya hatma ya Halima Mdee na wenzake. Taarifa iliyotolewa na CHADEMA inaeleza kuwa kwa sasa hatua inayofuata Chama kitawasiliana na […]

Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amewataka Watendaji wa Wizara ya Maji kutekeleza miradi kwa weledi, viwango na kuzingatia uadilifu. Mhe. Aweso amesema hayo wakati akifungua Mkutano wa wadau wa Sekta ya Maji katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano (wa AICC) Jijini Arusha, ambao unafanyika kwa siku mbili na kutaka Sekta Binafsi ipewe kipaumbele […]


Current track

Title

Artist