News

Bi. Stamili Endelea Kaloloma ambaye ni kikongwe wa miaka 119, mkazi wa Misegese wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro, ametelekezwa na watoto wake wapatao watano ambao hawataki kumtunza wala kumpatia mahitaji yake muhimu licha ya kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kupewa maagizo ya kumtunza kutokana na umri wake, badala yake wamemuacha apambane mwenyewe. Hali hiyo imemfanya […]

Vyombo vya habari nchini Korea Kaskazini, jana Jumapili, Januari 21, 2024 vimeripoti kuwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin anatarajiwa kuitembelea nchi hiyo hivi karibuni, kwa mwaliko wa Rais Kim Jong Un, hatua inayotajwa kuwa ni ishara kwamba ushirikiano kati ya viongozi hao wawili unaongezeka wakati vita vikiendelea nchini Ukraine na machafuko yakiongezeka Mashariki ya Kati. […]

MTANDAO wa Bayoanuai Tanzania umeshauri wakulima kulinda na kuendeleza kilimo cha asili ili kuendelea kuwa na uhuru wa matumizi ya mbegu za asili kwa usalama wa chakula na lishe. Mtaalam wa Mbegu kutoka katika mtandao huo, David Manongi amesema hayo katika warsha ya mbegu asili iliyofanyika mkoani Dar es Salaam. Amesema mbegu za asili ni […]

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi,ACP Janeth Magomi, amewaonya madereva kuacha tabia ya kuchezea mfumo wa Vehicle Truck Syteam  (VTS) kwani mfumo huo umewekwa kwa lengo mahususi la kusoma na kubaini mwendokasi wa magari ambapo kitendo cha kufanya hivyo ni kosa na atakaebainika atachukuliwa hatua za Kisheria. Kamanda Magomi ametoa onyo […]

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Jenista Mhagama. ametoa wito kwa watumishi walio chini yake kufanya kazi kwa kutegemeana na kushirikiana bila kutengeneza makundi. Ametoa rai hiyo mkoani Morogoro wakati akifungua kikao cha baraza la wafanyakazi la Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na uratibu kilicholenga kujadili taarifa ya bajeti […]

Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kupitia kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itifaki na Mambo ya Nje John Mrema kimethibitisha kupokea hukumu iliyotolewa Alhamisi tarehe 14 Disemba, 2023 uamuzi wa Mhe. Jaji Cyprian Phocas Mkeha juu ya hatma ya Halima Mdee na wenzake. Taarifa iliyotolewa na CHADEMA inaeleza kuwa kwa sasa hatua inayofuata Chama kitawasiliana na […]

Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amewataka Watendaji wa Wizara ya Maji kutekeleza miradi kwa weledi, viwango na kuzingatia uadilifu. Mhe. Aweso amesema hayo wakati akifungua Mkutano wa wadau wa Sekta ya Maji katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano (wa AICC) Jijini Arusha, ambao unafanyika kwa siku mbili na kutaka Sekta Binafsi ipewe kipaumbele […]

KUNA watu ambao wamejikuta hawakubaliki kwenye jamii zao. Jambo hilo ni baya na husababisha tatizo kubwa la kisaikolojia kwa mhusika. Hakuna mtu ambaye hapendi kukubalika, kupendwa na kushirikishwa kwa watu wanaomzunguka. Bahati mbaya ni kwamba, iwapo itatokea ukawa hukubaliki, hutafikiri au kuchunguza sababu za jambo hilo, badala yake utashikwa na hasira, utajisikia vibaya na kujitenga […]

Usiku wa kuamkia leo tarehe 10 Dec ndani ya mkoa ya Morogoro kumenyesha mvua kubwa Wilayani kilosa ambapo katika eneo la Manzese A wilayani humo imesababisha maji kuzingira katika makazi ya watu na kuharibu miundombinu. Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka amethibisha kutokea kwa mvua hizo huku akisema mbali na kuharibu miundombinu, shughuli […]

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bombambili iliyopo eneo la Bombambili Kata ya Kivule Wilaya ya Ilala jijini, leo wamefundishwa namna ya kupambana na ukatili wa kijinsia ikiwa ni sehemu ya siku 16 za kupinga ukatili duniani. Wanafunzi hao wamepata elimu hiyo kutoka kwa wanaharakati wa Kituo cha Taarifa na Maarifa (KC) cha Kata ya Kivule […]


Current track

Title

Artist