Rais Putin Kufanya Ziara Korea Kaskazini Kwa Mwaliko Wa Rais Kim Jong Un

Written by on January 22, 2024

Vyombo vya habari nchini Korea Kaskazini, jana Jumapili, Januari 21, 2024 vimeripoti kuwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin anatarajiwa kuitembelea nchi hiyo hivi karibuni, kwa mwaliko wa Rais Kim Jong Un, hatua inayotajwa kuwa ni ishara kwamba ushirikiano kati ya viongozi hao wawili unaongezeka wakati vita vikiendelea nchini Ukraine na machafuko yakiongezeka Mashariki ya Kati.

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amenukuliwa na Shirika la Habari la Urusi (TASS) akisema ratiba ya ziara ya Putin nchini Korea Kaskazini bado inajadiliwa kupitia njia za kidiplomasia na zitatangazwa baadaye.

Jumanne iliyopita, Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini, Choe Son Hui alikutana na Putin na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergey Lavrov jijini Moscow kujadili masuala yanayohusu Rasi ya Korea, Kaskazini mwa Asia na amani na usalama wa kimataifa.

Ziara ya Putin, Pyongyang itakuwa ni majibu ya ziara ya Kim aliyofanya Septemba, 2023 kwenye eneo la mashariki mwa Urusi, akitembelea kiwanda kinachozalisha ndege za kivita na kituo cha kurusha roketi miongoni mwa vituo vingine.


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *Current track

Title

Artist