MHAGAMA AHIMIZA KUTOKUWA NA MAKUNDI MAKAZINI

Written by on December 15, 2023

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Jenista Mhagama. ametoa wito kwa watumishi walio chini yake kufanya kazi kwa kutegemeana na kushirikiana bila kutengeneza makundi.

Ametoa rai hiyo mkoani Morogoro wakati akifungua kikao cha baraza la wafanyakazi la Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na uratibu kilicholenga kujadili taarifa ya bajeti ya 2023-2024 ya ofisi hiyo.

Waziri Mhagama amesema, kuna kila sababu ya kufanya maamuzi ya pamoja ya ushirikishwaji ili kuweza kupata mafanikio kwenye idara na vitengo, kama viongozi wenu wanavyofanya kazi vizuri kwa kushirikiana.

Aliendelea kusema kuwa hata kama inafikia wakati Mtendaji hayupo kwenye idara au kitengo kuwe kuna mtu anayeweza kufanya kazi kwa viwango na uwezo huo huo ili mambo yaweze kwenda vizuri.

“Tukifanya kazi kwa umoja na ushirikiano tukifanikiwa tuwe tumefanikiwa wote na tukianguka tujue tumeanguka wote na tujipange ili kujua sababu ya kuanguka na tuweze kujipanga.” Alibainisha.

Tagged as

Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *Current track

Title

Artist