CHADEMA YAPOKEA UAMUZI WA MAHAKAMA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kupitia kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itifaki na Mambo ya Nje John Mrema kimethibitisha kupokea hukumu iliyotolewa Alhamisi tarehe 14 Disemba, 2023 uamuzi wa Mhe. Jaji Cyprian Phocas Mkeha juu ya hatma ya Halima Mdee na wenzake.

Taarifa iliyotolewa na CHADEMA inaeleza kuwa kwa sasa hatua inayofuata Chama kitawasiliana na Mawakili wake ili kutafakari hatua za kuchukua ikiwa ni pamoja na kumkumbusha Spika wa Bunge kuhusu utekelezaji wa uamuzi wa Kamati kuu ya Chama wa tarehe 27 Novemba, 2020 kwani Mahakama imethibitisha kuwa walishafukuzwa uanachama kihalali na taratibu zote zilifuatwa. #planetfmtz

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top