KOCHA WA SENEGAL SASA FRESH, BAADA YA KULAZWA MCHEZO NA CAMEROON ULIPOISHA

Kocha wa timu ya taifa ya Senegal, Aliou Cisse alipata matatizo ya kiafya, akawahishwa hospitalini kufuatia ushindi dhidi Cameroon, lakini sasa anaendelea vyema baada ya matibabu.

Senegal waliendeleza mwanzo mzuri wa kutetea taji lao la Mataifa ya Afrika kwa ushindi wa mabao 3-1 na kutinga kibabe hatua ya 16 Bora.

Hata hivyo Cisse alipata tatizo la kiafya na akapatiwa matibabu katika hospitali ya mjini Yamoussoukro ambako alilazwa usiku mzima. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 47 baada ya hapo aliruhusiwa kutoka hospitalini na kurejea kikosini kwake.

Taarifa ya shirikisho la soka la Senegal ilisema: “Vipimo alivyofanyiwa vimemhakikishia yuko sawa na amerejea kundini. Anaendelea vyema,” msemaji wa timu ya Senegal, Kara Thioune aliongeza.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top