Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi,ACP Janeth Magomi, amewaonya madereva kuacha tabia ya kuchezea mfumo wa Vehicle Truck Syteam (VTS) kwani mfumo huo umewekwa kwa lengo mahususi la kusoma na kubaini mwendokasi wa magari ambapo kitendo cha kufanya hivyo ni kosa na atakaebainika atachukuliwa hatua za Kisheria.
Kamanda Magomi ametoa onyo hilo, Desemba 20,2023 wakati akizungumza na madereva, makondakta na mawakala katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani alipokuwa mkoani Shinyanga.
Aidha, Kamanda Magomi akiwa ameambatana na Mabalozi wa Usalama Barabarani (Road Safety Ambassadors) ametumia fursa hiyo kuwaomba abiria kuendelea kutoa taarifa kupitia namba za simu ambazo zipo katika vipeperushi walivyogawiwa na zilizopo kwenye magari pindi pale dereva atakapokiuka Sheria za Usalama barabarani na kufanya vitendo vingine vya ukiukwaji wa sheria ikiwa pamoja na kuendesha chombo cha moto kwa mwendokasi.