BENCHIKHA KUTUPA KETE YAKE YA KWANZA LIGI KUU

Written by on December 15, 2023

Kocha mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha baada ya kutoka Ligi ya Mabingwa, leo atakuwa na mtihani mwingine kwenye Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar utakaochezwa leo saa 10:00 jioni katika uwanja wa Uhuru.

Benchikha amekaa benchi kwenye mechi mbili za Simba dhidi ya Jwaneng Galaxy 0-0 na Wydad ambayo walifungwa 1-0.

Katika mechi hizo mbili Simba ikiwa chini ya Benchikha haijafunga bao lolote lile kwenye Ligi ya Mabingwa hivyo kinachosubiliwa ni kuona namna ambavyo ataanza Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar.

Michezo minne iliyopita kwenye Ligi Kuu pindi timu hizo zilipokutana, Simba imeshinda michezo miwili, sare moja na kupoteza mchezo mmoja.

Tagged as

Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *Current track

Title

Artist