KILOSA YANYESHA MVUA KUBWA USIKU WA KUAMKIA LEO

Written by on December 10, 2023

Usiku wa kuamkia leo tarehe 10 Dec ndani ya mkoa ya Morogoro kumenyesha mvua kubwa Wilayani kilosa ambapo katika eneo la Manzese A wilayani humo imesababisha maji kuzingira katika makazi ya watu na kuharibu miundombinu.

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka amethibisha kutokea kwa mvua hizo huku akisema mbali na kuharibu miundombinu, shughuli za usafiri na usafirishaji zimekwama na magari yakiwa mbioni kusombwa, pia imefanya Kilosa pawe kama Kisiwani kutokana na Watu kushindwa kuingia na kutoka ambapo pia barabara ya kutoka Kilosa kwenda Mikumi imefungwa kwa muda.

Amesema ya kwamba maji hayo yanayotokea daraja la Mto Mkondoa na daraja la mazinyungu kwa kasi hadi kwenye makazi ya Watu baada mito kuhama katika njia zake za asili kwenye baadhi ya maeneo.

“Pamoja na madhara kwa Wananchi kupata athari kwenye makazi yao bado hatujawa na takwimu sahihi ya madhara hayo, madhara makubwa yametokea kwenye barabara , tupo kama Kisiwani hatuna mawasiliano wanaotoka Dumila kuja Kilosa hauwezi kuingia Kilosa Mjini, wanaotoka Kilosa Mjini kwenda Mikumi tumezuia barabara hiii kutokana na daraja linalounganisha pande mbili limelika kwa kiasi kikubwa sana kutokana na nguvu kubwa ya maji kwenye Mto Mkondoa”

Huku akiongeza kuwa “Kamati ya Usalama tupo hapa ili kuhakikisha tuna-control hali hii ili Wananchi wabaki salama wakati tukifikiria namna ya kuwasaidia Wahanga, tunamshukuru Mungu hakuna madhara ya Binadamu hadi sasa”


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *Current track

Title

Artist