HATMA YA SIMBA IPO KWA MKAPA UONGOZI WAFUNGUKA HAYA KUHUSU WYDAD

Written by on December 11, 2023

Klabu ya Simba imesema kuwa hatima yao ya kufuzu hatua ya makundi na kwenda robo fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika iko mikononi mwao, Desemba 19, 2023 watakapokutana na mpinzani wao, Wydad Casablanca.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally baada ya kumalizika kwa mchezo wa kwanza uliopigwa Marrakech nchini Misri juzi Jumamosi na Simba kukubali kichapo cha bao 1-0 dakika za lala salama.

“Kwenye kilele cha ubora wetu, tumepoteza mchezo. Kazi nzuri wachezaji wetu mmepambana na kuvuja jasho kwa ajili ya timu yetu lakini dakika za nyongeza zimekua katili kwetu.

“Hatma yetu ipo mikononi mwetu Desemba 19, tunamkaribisha Wydad kwenye Tanuri la Moto Benjamin Mkapa, tutakachomfanya tunajua sisi,” amesema Ahmedy Ally.

  1. ASEC Mimosas – pointi 7
  2. Jwaneng Galax – pointi 4
  3. Wydad Casablanca – pointi 3
  4. Simba SC – pointi 2.

Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *Current track

Title

Artist