RAIS WA KLABU AMSHUSHIA NGUMI NZITO MWAMUZI WA MCHEZO

Written by on December 12, 2023

Mwamuzi wa Ligi Kuu ya Uturuki apingwa ngumi usoni na rais wa klabu ya Ankaragucu kwenye mchezo uliozikutanisha klabu za Rizespor dhidi ya Ankaragucu, usiku wa Jumatatu.

Tukio hilo la kushangaza lilijiri baada ya Rais wa Ankaragucu, Faruk Koca, kuvamia uwanjani baada ya mchezaji wa Rizespor, Adolfo Gaich, kufunga bao la kusawazisha dakika ya 97 na kumpiga ngumi mwamuzi Halil Umut Meler aliyeanguka chini, na kusababisha fujo kubwa kuibuka.

Baada ya kuanguka mwamuzi huyo alipigwa teke la kichwani na mtu mwengine ambaye hakufahamika kwa jina, kabla ya maafisa usalama kumuongoza mwamuzi huyo kwenye vyumba vya kubadilishia nguo akiwa na uvimbe jichoni, huku Rais huyo, (Koca) akishikiliwa na polisi wa mjini Ankara.

Kufuatia tukio hilo, Rais wa Shirikisho la Soka la Uturuki ametangaza kusimama kwa shughuli zote za mpira wa miguu nchini humo kwa muda usiojulikana.


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *Current track

Title

Artist