PAPA FRANCIS ALAZWA HOSPITAL KUTOKANA NA MAAMBUKIZI YA MAPAAFU

Written by on November 28, 2023

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis (86) anapatiwa matibabu ya ugonjwa uliojitokeza kwenye mapafu yake.

Kutokana na hali hiyo, Kiongozi huyo amelazimika kuahirisha mikutano yake na hafla kadhaa.

Taarifa kutoka Vatican, ambapo ndio Makao Makuu ya Kanisa Katoliki, zimeeleza kuwa hali hii ya kiafya inamletea Papa taabu katika mfumo wa upumuaji, hata hivyo hana nimonia wala homa.

Hata hivyo, bado Papa Francis anapanga kusafiri kwenda Falme za Kiarabu kutoa hotuba kuhusu mabadiliko ya tabia nchi katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa COP28 unaotarajia kufanyika Novemba 30 hadi Desemba 12.

Jumapili iliyopita Kiongozi huyo alisema kuwa hivi karibuni amekuwa hajisikii vizuri na amelazimika kufuta ratiba yake ya kila wiki ya kuwasalimu watu kupitia dirisha la St.Peter’s Square.


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *Current track

Title

Artist