CHAMA KALIAMSHA HUKO NDANI YA SIMBA

Written by on December 6, 2023

CLATOUS Chama, mwamba wa Lusaka ameanza kujipata taratibu baada ya kuonyesha ubora uliokosekana kwa muda mrefu ndani ya uwanja.

Chini ya Roberto Oliveira, mchezo wa mwisho kufanya umwamba ilikuwa dhidi ya Power Dynamos alipofunga mabao mawili, ubao uliposoma Power Dynamos 2-2 Simba baada ya hapo hakuwa kwenye ubora wake.

Ikumbukwe kwamba alikuwa ndani ya Uwanja wa Mkapa, Novemba 5, 2023, ubao uliposoma Simba 1-5 Yanga, Simba 1-1 Namungo. Kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas alianzia benchi na alipoingia bado hakufurukuta.

Chini ya Abdelhak Benchikha, mrithi wa Oliveira mchezo wake wa kwanza ilikuwa Desemba 2, dhidi ya Jwaneng Galaxy alipoanzia benchi, aliingia dakika ya 62 akichukua nafasi ya Willy Onana.

Katika dakika 28 alizocheza alionyesha kitu kwenye miguu yake ambapo alipiga zaidi ya pasi 11 na aliokoa hatari dakika ya 65. Katika shuti lake la dakika ya 90 liligonga mwamba ikiwa ni hatari ya mwisho kutengenezwa kwa Simba.

Hivyo kwa kasi aliyoanza nayo ugenini ikiwa ataendelea hapo kuna uwezekano kupenya kikosi cha kwanza huku mshikaji wake, Luis Miquissone mambo yanaonekana bado magumu kwake.

Kikosi cha Simba kipo Morocco kwa sasa kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad unatarajiwa kuchezwa Desemba 9 2023.

Miongoni mwa nyota waliopo kwenye kikosi hicho ni pamoja na Chama, Mzamiru Yassin, Ayoub Lakred.


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *Current track

Title

Artist