BENCHIKHA AOMBA USHIRIKIANO KWA WANASIMBA WOTE

Written by on November 28, 2023

Kocha mkuu mpya wa timu ya Simba Sc Abdelhak Benchikha amezungumza kwa hisia na waandishi wa habari Nina furaha kubwa kuwepo hapa.

Tangu nilipoanza kuwasiliana na viongozi nilikuwa na shauku ya kuja. Jambo kubwa ambalo naomba ni mashabiki kutupa ushirikiano na naamini kupitia hilo tutafanikiwa pamoja.”

“Kuna mambo mengi ambayo tayari nayajua na nimekuja na mikakati ambayo taifanyia kazi. Kuhusu wachezaji tajua zaidi nikishaanza kazi, kuhusu mashindano ya ndani na kimataifa yote ni muhimu. Mimi ni mpambanaji na nitapambana hadi tutafika.”

“Mafanikio yatajengwa na Wanasimba wote hilo ndio muhimu zaidi. Kwa wachezaji sitaangalia majina bali anayefanya vizuri, kiwango cha mchezaji ndio kitafanya nimtumie.”


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *Current track

Title

Artist